MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI WA KATA WAASWA KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA KAZI ZAO

Na OR – TAMISEMI

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kubadilishana uzoefu wa kazi na changamoto wanazozipitia kwa kujua ni namna gani wanaweza kuzitatua kwa pamoja.

Mhe. Shigela ameyasema hayo Aprili 28, 2024 wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata wa mkoa wa Geita yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Mhe. Shigela amesema kutatua changamoto ni pamoja na kujibu barua za wananchi kwa wakati ili kupunguza malalamiko na kero zinazowakabili kama sehemu ya kuimarisha Utawala Bora kwenye maeneo yao.

“Watendaji Kata na Maafisa Tarafa zingatieni utawala bora ili kuleta maendeleo katika Kata na Tarafa zenu” alisema Mhe. Shigela

Aidha, amesema Mtendaji wa Kata na Afisa Tarafa ndio wasimamizi wa miradi yote inayoendelea katika Kata na Tarafa na miradi yote inayoanzishwa na sekta zote zinatakiwa kutolewa taarifa kwa maafisa hao pamoja na kuwepo kwa uwazi katika utekelezaji wake.

Related Posts