Na MWANDISHI WETU.
Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi
cheti cha udhamini Bi. Lulu Mengele, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma
wa NSSF kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, kwa kuwa miongoni mwa wadhamini wa
Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF), uliofanyika tarehe 29 Aprili, 2024 jijini Dodoma.
Katika
mkutano huo ambao uliofunguliwa na Mhe. Dkt. Biteko, amaesema Serikali
ya awamu ya sita inathamini mchango mkubwa unaotolewa na vyombo vya
habari nchini.
Akitoa elimu ya hifadhi ya jamii katika mkutano
huo, Bi. Lulu Mengele amesema NSSF inaendelea kufanya vizuri kwenye
sekta ya hifadhi ya jamii na kuwa imeboresha mifuko ya TEHAMA ambayo ni
rahisi na rafiki kwa wanachama ambao wanaweza kuangalia taarifa zao
mbalimbali zikiwemo za michango bila ya kulazimika kufika katika ofisi
za NSSF. Aidha, amewataka waajiri wa sekta binafsi kuhakikisha
wanawasilisha michango ya wafanyakazi wao kila mwezi kwani hilo ni takwa
la kisheria.