MEI MOSI YAFANA ARUSHA, RC MAKONDA ALIA NA UBOVU WA BARABARA

  

Na. Vero Ignatus Arusha

Maadhimisho
ya sherehe za mei mosi kit aifa yamefanyika Mkoani Arusha ambapo
yamekuwa na zaidi ya waandamanaji 7000 mbali na wananchi ambao
walioshiriki katika maadhimisho hayo.

Akitoa salam za mkoa mkuu
mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda aliweza kumuomba Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kufikisha salamu kwa
Rais wa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakazi wa Arusha wanatambua mchango
wake hasa kwenye sekta ya utalii.

“Wananchi wa jiji la Arusha na
mkoa wa Arusha kwa ujumla wake wanayo furaha kubwa sana kwa kazi kubwa
aliyoifanya ya ‘Royal Tour’ na hivi tunaelekea kwenye high season hivyo
tunategemea kupata watalii wengi sana, na kwetu sisi wananchi wa kila
kada awe ni muuza mchicha, awe ni Bodaboda, awe ni mtu anayelima nyanya,
Bilinganya nk anafaidika na utalii kwa kuwa Hoteli zikijaa na yeye
anapata nafasi ya kuuza na hatimaye anaendesha maisha yake” Alisema
Makonda

Sambamba na salam hizo Makonda aliweza kutoa ombi lake
kwa mgeni Rasmi kwamba Rais kwamba jiji hilo Lina mchango makubwa wa
wadau wa utalii, hivyo ameomba kusaidiwa kutengeneza barabara ya Jiji
hilo,kwani barabara siyo nzuri na wananchi wanashindwa kufanya kazi zao
kwa usahihi, lna kwa usalama

“Tunataka kufanya utalii wa Jiji
letu kwa lands nzima ya kaskazini tumekubaliana kuanzisha kituo ki moja
cha uwekezaji (one stop Center) Jiji la Arusha.”

Makamu wa Rais
Dkt Philip Isdory Mpango akijibu risala ya TUCTA alisema kuwa kuhusu
nyongeza ya mishahara mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilipandisha kima
cha chini cha mishahara kwa asilimia 23.3 kutoka shilingi 300,000 (laki
tatu) hadi shilingi 370,000 kwa mwezi, lengo la kutoa nyongeza kwa
kiwango hicho ilikuwa ni kuwezesha watumishi wenye mishahara ya kima cha
chini kumudu gharama za maisha kwa kadri inavyowezekana

Dkt
Mpango amesema makundi mengine ya watumishi ambayo yaliguswa na ongezeko
hilo la mishahara kwa viwango tofauti kwa kuzingatia ukomo wa bajeti wa
mishahara iliyotengwa, huku akiendelea kusema kuwa serikali itaendelea
kuhuisha viwango vya mishahara kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi na
kibajeti pamoja na ujuzi na utendaji wa waajiriwa, misingi hii ni muhimu
ili kuepuka kuchochea mfumuko wa bei kuhatarisha uhimilivu wa deni la
Taifa na athari nyingine kwenye uchumi wa Taifa kwa ujumla.

“Haya
yote lazima yazingatiwe katika mchakato wa kuongeza mishahara na
hususani katika kipindi ambapo uchumi wa Dunia umekumbwa na misukosuko
mingi ikiwemo vita baina ya Urusi na Ukraine, vita vya mashariki ya kati
inayohusisha Israel, Palestina, Lebanon, Syrian, Iran na Yemen” Alisema
Dkt. Mpango

Dkt. Mpango. Amesema Vita hivyo vimepelekea
kuvurugika kwa mfumo wa ugavi na kupanda sana kwa bei ya mafuta, mbolea,
chuma na chakula, na kama hiyo haitoshi Dunia imekumbwa na majanga
mengine ikiwemo mvua kubwa na maporomoko ya udongo ambayo yamesababisha
uharibifu mkubwa wa miundombinu, magonjwa na hata vifo.

“Changamoto
zote hizi zimeathiri pia uchumi wetu, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan mama wa Taifa ameniagiza niwaambie wafanyakazi wa Tanzania
kuwa endapo hali hii itadumu wafanyakazi wawe na matumaini kwamba
atasema jambo hivi karibuni” -Dkt. Mpango

Kawa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kassim
Majaliwa amewapongeza wakazi wa Mkoa wa Arusha kwa hamasa na maandalizi
ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani leo Mei Mosi, 2024.

Aidha
ameahidi kuwa Ofisi Yake itaendelea kishriikiana na vyama hya
wafanyakazi kuangalia namna gani wanaweza kutatua changamoto mbakimbali
zitakazojitokea.


Related Posts