RC MALIMA ATAKA WANANCHI KUPIMA AFYA WAKATI WA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kushiriki kupima Afya zao wakati wa Kambi Maalum ya Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassani (Outreach Services) ili kukabiliana na magonjwa waliyonayo au yale ambayo wanayo bila ya wao kujua.

Mhe. Malima ametoa wito huo wakati akiongea na waandishi wa habari akitoa taarifa ya kambi hiyo itakayofanyika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuanzia Mei 6 hadi 10 2024.

 

Mkuu wa Mkoa Adam Kighoma Malima amesema, kambi hiyo maalum inayojulikana kama ni ya kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodomd, Iringa, Singida, Pwani na wenyeji Morogoro itwapokea wanchi wote wanaotaka kupata huduma hiyo maalum na yenye gharama nafuu kwa wananchi kutoka mikoa hiyo iliyotajwa hapo juu.

Aidha, amesema, Kambi hiyo inakadiriwa kutoa huduma za afya kwa wagonjwa 200 na kufanya upasuaji kwa wagonjwa 100 kwa siku watakazokuwepo kambini ambapo huduma zote za kumuona daktari zitatolewa kwa Tsh. 5000 pekee, hivyo wananchi wenye matatizo mbalimbali na wanaotaka kujua afya zao na kutaka ushauri watatakiwa kufika kambini hapo.

 

Sambamba na hilo, Mhe. Adam Malima amewataka Wakuu wa Wilaya zote na Wakurugenzi kuhamasisha wananchi katika maeneo yao na kutafuta namna bora ya wagonjwa kuweza kujisajili na kufika katika kambi hiyo ili kupata huduma hiyo.

Hata hivyo amebainisha njia zitakazotumika katika kujisajiri mapema kabla ya siku au tarehe za kupata huduma hiyo ikiwemo wananchi kwenda kuwaona Wakuu wa Wilaya zao, kuwaona Wahe.wabunge wao na Wakurugenzi wa Halmashauri zao

 

Awali, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro Dkt. Kusirye Ukio amesema kuwa Kambi hiyo itakuwa na Madaktari 54 ambao wanatoka katika Mikoa minne (4) ikiwa na lengo la kufikisha huduma kwa wananchi sambamba na kutoa ujuzi kwa madaktari waliokaribu na eneo la tukio, hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto nyingi za Afya kwa wananchi wa Mikoa Pwani, Morogorom Iringa, Singida na Dodoma.

 

Related Posts