SERIKALI YAPOKEA USHAURI WA TUCTA KUIWEZESHA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI CMA

Serikali imesema imepokea ushauri wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA, la kuiwezesha Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA kwa kuipatia vitendea kazi pamoja na kuongeza idadi ya Wasuluhishi na Waamuzi ili kuboresha huduma zake.

Ameyasema hayo makamu wa Rais Mhe. Dkt. Isdori Mpango wakati akijibu hoja za hotuba iliyowasilishwa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA, katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika mkoani Arusha kitaifa leo Mei 01,2024.

Makamu wa Rais amesema serikali kwa kutambua umuhimu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA na ushauri wa TUCTA itaiwezesha CMA kupata vitendea kazi pamoja na kuongeza nguvu kazi ili kuboresha huduma za Tume ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari kwaajili ya usafiri ili kuwafuata walalamikaji wa migogoro ya kikazi walioko mbali na Ofisi za Tume hasa kwa ngazi ya wilaya ambako hakuna huduma hiyo.

Naye katibu mkuu wa , shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA, Bw.Henry Mkunda wakati akiwasilisha hotuba ya TUCTA katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani amesema kwakuiwezesha Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA, itasaidia kuimarisha ufanisi na wafanyakazi kupata haki zao hasa walioko Katikati ngazi ya wilaya ambako huduma za Tume hazipatikani.

Vilevile TUCTA imesema migogoro ya watumishi wauma iweze kurejeshwa na kushughulikiwa na CMA kwani itahasaidia kutatua migogoro kwa haraka.

Kwaupande wake, rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA, Tumaini Nyamhokya amesema, kwa kuiwezesha Tume ya Usuluhishi na Uamuzi itasaidia kutatua changamoto ya migogoro ya wafanyakazi katika mikoa na ngazi ya wilaya ambako kumeonekana kukosa huduma hiyo hivyo kuwanyima wananchi haki yao.

Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA ni taasisi huru inayoshughulika na utatuzi wa migogoro ya Kikazi Tanzania bara, baina ya Mwajiri,mwajiriwa pamoja na vyama vya wafanyakazi.

Related Posts