WANACHI 3666 KATA YA FUKAYOSI KUNUFAIKA NA MRADI UNAOTEKELEZWA NA RUWASA

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

Wananchi wapatao elfu 3666 katika kijiji cha Kidomole pamoja na vitongoji vyake mbali mbali vilivyopo katika kata ya Fukayosi Wilayani Bgamoyo Mkoa wa Pwani wanatarajia kuondokana na changamoto ya usumbufu wa majii fikapo mwezi Mei mwaka huu baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji ambao utakuwa ni mkomboz mkubwa kwa wananchi hao.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa wakala wa Usambazaji wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Bagamoyo James kionaumela wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Godfrey Mnzava kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo ambapo alisema kwa sasa upo katika hatua za mwisho kwa ajili ya upanuzi.

Meneja huyo alibainisha kwamba unatekelzwa chini ya mkandarasi mzawa AM&Partiner Limeted na Building Contractors kutoka jijini Dar es Salaam na kwamba kwa mujibu wa mkataba huo mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei 11 mwaka huu.

Alifafanua kwamba katika upanuzi wa mradi huo pia unakwenda sambamba na ujenzi wa tibio la maji katika eneo la Saadan na kwamba mradi huo umegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 603 ambazo ni fedha kutoka katika mfuko wa maji( NWF)

Meneja huyo alibainiha kwamba utekelezaji wa mradi huo ulianza rasmi mnamo tangu Mei 11 mwaka 2023 na pia utaweza kuzinufaisha kaya zipatazo 796 kutoka kata ya Fykayosi pamoja na vitongoji vyake wananchi wataweza kuondokana na changamoto ya maji na hatimaye kupata huduma ya maji safi na salama.

Pia alisema kuwa katika kutekeleza mradi huo umeweza kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana wa lika mbali mbali wapatao 50 ambao kwa sasa wameweza kujipatia kipato halali na kujikwamua kiuchumi.

Meneja huyo alibainisha kwamba katika eneo la kijiji cha Kidomole utekelezaji wa mradi huo umefikia kwa kiwango cha asilimia 90% ikiwa ni pamoja na ujenzi wa tanki kubwa lenye ujazo wa lita elfu 50,000 kwenye mnara wa mita 12.

Katika hatua nyingine Meneja huyo alitoa shukrani za dhati kwa Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anatenga fedha katika kuboresha sekta ya maji kwa vitendo lengo ikiwa ni kuwapatia huduma wananchi ya maji safi na salama.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava pamoja na wakimbiza mwenge wenzake wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kukubaliana kwa pamoja kuupitisha pamoja na kuwapongeza Ruwasa kwa kazi nzuri ambazo wanazifanya katika kuwapelekea huduma ya maji wananchi.

Alisema kwamba huduma ya maji ni muhimu sana kwa wananchi hivyo Ruwasa waendelee kuchapa kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatekeleza miradi ya maji kwa kiwango ambacho kinastahili kulingana na fedha ambazo zinatolewa na Rais.

Related Posts