Na Pamela Mollel Arusha
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amepongeza juhudi kubwa iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Paul Makonda katika maandalizi ya siku ya wafanyakazi Dunia (MEI MOSI)zinazofanyika Kitaifa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoa Arusha
Ameyasema hayo leo katika maandimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo amesifu kazi kubwa iliyofanywa na Makonda kuhamasisha makundi mbalimbali kuhudhuria maadhimidho hayo
“Nimeshiriki Maadhimisho mengi sanaa ila Arusha imetia fora kubwa maadhimisho haya nimpongeze sana Mh Makonda lakini pia na wananchi wa Arusha kwa kujitokeza kwa wingi”alisema Majaliwa
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Poul Makonda amesema Mkoa huo ni shwari na tulivu hivyo wageni mbalimbali wanakaribishwa kufika katika jiji hilo
Pia ameomba miundombinu ya barabara katika jiji hilo kukarabatiwa ili kuharakisha shughuli za wananchi kusonga mbele kwa kuwa hali ya barabara za Arusha haziridhishi kabisa.