CSSC YAGAWA VITABU VYENYE THAMANI YA SH MILLION 60 KWA VYUO VYA FAMASI NCHINI

 

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akigawa vitabu mara baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC, Peter Maduki,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa huduma za Afya kutoka Christian Social Services Commission (CSSC) Dkt.Josephine Balati,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Mkuu wa Miradi, Ukanda wa Afrika kutoka shirika la action medeor e.v,Bi.Susanne Schmitz,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Baadhi ya Washiriki wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah (hayupo pichani),wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akigawa vitabu mara baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu

 Shirika la Christian Social Services Commission (CSSC) kwa kushirikiana na shirika la action medeor e.v la nchini Ujerumani wamefanya mkutano wa mwaka ambao umewakutanisha wadau wa famasi nchini Jijini Dodoma.

Kwa pamoja wameshiriki kujadili mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka mitatu ya awamu ya pili ya mradi wa Multi-actors Partnership for Quality Pharmaceutical services (MAP-QPS). 

MAP-QPS ni mradi unaoshirikisha wadau mbalimbali wenye lengo la kuboresha huduma za kifamasia Tanzania. Baadhi ya wadau ni CSSC, action medeor e.v, Wizara ya Afya, Baraza la Famasi, Vyuo vya famasi (vyuo vya kati na vyuo vikuu), Chama cha Wafamasia, Chama cha wanafunzi wa famasi, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi, Tume ya vyuo vikuu, Hospitali za mikoa na Hospitali za Rufaa naTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mafanikio ambayo yamepatikana katika awamu ya pili ya mradi huu ni: kuboresha mafunzo ya famasi Tanzania, kutengeneza mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kutathmini na kuboresha mafunzo (CQIMS), kutengeneza jukwaa la kidigitali (Digital Learning Platform-DiLPHAS), kwa ajili ya kurahisisha kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa famasi kutoa mafunzo ya huduma tabibu za kifamasia (Clinical Pharmacy Services) kwa wafamasia wafanyakazi katika hospitali 29 zikiwemo za kanda, mikoa, rufaa na hospitali za kibingwa, kutoa mafunzo ya mbinu za ufundishaji (Teaching Methodology and Assessment) kwa wakufunzi 200 wa vyuo vya kati vya famasi, kukarabati na kutoa vifaa vya maabara kwa chuo cha Afya na sayansi shirikishi Mpanda, kuboresha miundombinu na kutoa vifaa vya maabara ya chuo kikuu cha RUCU, Kuwezesha kufanyika mapitio ya mitaala ya Famasi na kwezesha upatikanaji wa vitabu 1800 vya rejea kwa vyuo vinavyotoa mafunzo ya famasi.

Sambamba na hayo, Mkutano huu umezindua rasmi mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kutathmini na kuboresha mafunzo katika vyuo vya afya nchini. 

Aidha katika mkutano huu, CSSC imetoa vitabu vya ziada vyenye thamani ya shillingi Milioni 68 vilivyoandaliwa kwa ajili ya mafunzo ya famasi. Vitabu hivyo vimegawiwa kwa vyuo takribani 100 vinavyotoa mafunzo ya famasi. 

Akiongea wakati wa kukabidhi vitabu hivyo mkurugenzi wa CSSC, Peter Maduki alisema, “Vitabu hivi vimenunuliwa kutoka kwa waandishi wazawa wa nchini kwetu Tanzania na vitanufaisha wanafunzi wa kada ya famasi na vitawasaidia kuongeza ujuzi na uelewa wao wa masomo ya famasi ili kuboresha viwango vya mafunzo na wataalamu bora wa famasi.”

Akikabidhi vitabu hivyo Naibu Mganga Mkuu wa Serikali, Ziada Sellah amesema “ Wakufunzi na wataalamu wa famasi tuendelee kuongeza ujuzi wetu ili tuweze kufanya kazi kwa uweledi na tuchangie ukuaji wa sekta ya afya.”

Katika kipindi cha miaka mitatu ijayo mpaka 2026 tunaingia katika awamu ya tatu ya Mradi ambao tutashirikiana na Chuo Kikuu Cha sayansi na Afya shirikishi cha Muhimbili kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo wafamasia waliopo kwenye ajira kwenye hospitali za kanda, rufaa na maalumu ya namna bora ya kutoa huduma tabibu za kifamasia. 

Related Posts