Kila mtumishi kwenye ofisi yake anunue gari “Hakuna haja ya kusubiri lift ya mtu”:

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameagiza watumishi wote kwenye ofisi yake kununua magari binafsi ili kupunguza wivu wa kutumia magari ya serikali.

 

Mtaka ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi kwenye sherehe ya wafanyakazi (Mei Mosi) iliyofanyika kimkoa kwenye uwanja wa sabasaba mjini Njombe

“Nimewaambia watumishi kuwa magari sasa hivi ni milioni nane mpaka kumi na mbili,nunua ka IST kako weka mafuta ya elfu ishirini unaenda ofisini utapunguza roho mbaya kugombania magari ya ofisi wala hutawaza kunyang’anya haki ya mtu na nimewaambia watumishi wa RS watumishi mko wa ngapi themanini gari zipaki themanini hakuna haja ya kusubiri lift ya mtu”amesema Mtaka

Vile vile Mtaka amesema gari ya mkuu wa mkoa ana haki kupanda mtu yeyote kwa kuwa gari hiyo imetokana na kodi za wananchi

Gari langu mkuu wa mkoa ni gari la kodi za Watanzania yeyote atapanda, kwanini gari la ofisi likutoe roho mpaka umnunie mtu sasa wewe gari ni STL,DFP inakutoa roho mpaka uchukie watu”alisema Mtaka

 

Related Posts