RAIS DK.MWINYI AIFUNGUA SKULI YA SEKONDARI UTAANI WETE-PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa Skuli ya ghorofa ya Sekondari Utaani ni utekelezaji wa ahadi ya serikali aliyoitoa baada ya tukio la moto iliyoteketeza skuli ya awali iliyokuwa na madarasa 11 na kuahidi kujenga skuli bora zaidi ambayo kwasasa ina madarasa 41.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo leo tarehe 1 Mei 2024 alipofungua Skuli ya Sekondari Utaani iliopo Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba na kujengwa upya na serikali baada ya kupata ajali ya moto mwezi machi mwaka 2022.

Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itajenga Dahalia kubwa ya kisasa itakayoendana na hadhi ya skuli hiyo.

Related Posts