Wasusa kumzika marehemu wakidai ameuawa kishirikina

Njombe

Wananchi wa mtaa wa Muungano halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wamegomea kuuzika mwili wa kijana Elisha Nyalusi (35) wakidai kifo chake kimesababishwa na imani za kishirikina huku wakimtuhumu baba yake na kutaka arudishwe akiwa hai.

Wananchi hao akiwemo Nickson Nywage,Eliud Mwenda na Salima Mangula wamesema wamegomea kuuzika mwili huo kutokana na vijana wenzao wengine watatu kupoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha na kueleza kuwa vifo vyao vyote vimetokea tarehe za mwisho wa mwezi.

“Nadhani kulikuwa na mzozano wa shamba baadaye baba yake akamtuma akanunue dawa (roud up) ndipo alipodoka likimsokota tumbo kwa hiyo tumesusia kwasababu tumeumia yani sasa mwaka huu wametoka vijana wanne tayari kwa hiyo haturidhiki tunataka amrudishe tunaona vijana wenye nguvu wanapotea”wamesema wananchini

Hata Hivyo Baba wa kijana huyo aliyepoteza  maisha mwenye umri wa miaka 72  amekana kujihusisha na  Masuala ya imani za kishirikina na kueleza kuwa hakuwa na mgogoro wowote na mtoto wake kwani  na ndiye aliyekuwa akimtunza.

“Mtoto wangu tulishamalizana na alinunua shamba kwangu mbele ya mwenyekiti na shamba nilimkabidhi kwa hiyo tulikuwa hatuna changamoto yeyote na huyu mtoto wangu ndio aliyekuwa ananitunza”amesema baba Mzazi

Mwenyekiti wa mtaa wa Muungano Amelye Mteleke amekiri wananchi kugomea kuuzika mwili wa kijana huyo ambapo amesema tayari baba mzazi wa kijana huyo amechukuliwa na Polisi kwa ajili ya usalama wake.

“Inaonekana kuna maneno ya uchochezi yanayoashiria ushirikina amekuwa akiyatamka kwa hiyo vijana wote pamoja na wazee wamekasilishwa wakasema sasa we mzee utazika mwenyewe na familia yake inamtuhumu kwamba ni mshirikina”amesema Mteleke.

Related Posts