Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Helium One, Lorna Blaisse na Mkurugenzi wa Fedha na Biashara, Graham Jacobs wakifuatilia Bunge la Bajeti ya Wizara ya mwaka 2024/2025 lililopitishwa na Bunge. Helium One ilifikisha asilimia 4.7 ya heliamu kutoka kwenye kisima chao cha Itumbula Magharibi-1 mwezi Februari kilichopatikana kusini mwa Rukwa. Kampuni hiyo itaanza mwendelezo wa shughuli za majaribio ya kisima mwezi Julai.