NAIBU WAZIRI PINDA AKABIDHI BAISKELI KWA WALEMAVU KAVUU

Na Munir Shemweta, MLELE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda amekabidhi baiskeli za walemavu wa miguu ikiwa ni jitihada za kuwasaidia watu wenye ulemau.

Mhe, Pinda amekabidhi baiskali tarehe 2 Mei 2024 wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kirida katika Kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi.

Baiskeli iliyokabidhiwa kwa mlemavu Bi. Adela John mkazi wa Kirida ni sehemu ya baiskeli nne zilizotolewa kwa walemavu wa miguu wa jimbo la Kavuu ikiwa ni njia ya kuwasaidia usafiri wa kuwawezesha kwenda maeneo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hiyo, Mbunge wa jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Pinda amesema kuwa, anatambua adha wanayoipata walemavu wa miguu katika jimbo lake ndiyo maana ameona ipo haja ya kuwapatia baiskeli zitakazowasaidia kwenda katika shughuli zao.

‘’Ni matumaini yangu kuwa baiskeli hii itakuondolea adha uliyokuwa ukiipata na kwa sasa itakusaidia sana wakati wa kwenda katika shughuli zao mbalimbali’’ alisema Mhe, Pinda.

Mapema kwenye mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi, Mhe, Pinda aliwaeleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, pamoja na kukabiliwa na majukumu ya uwaziri lakini amekuwa akifanya juhudi ya kuwatumikia katika kuwaletea maendeleo.

Amezitaja juhudi hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, zahanati na vituo vya afya, madaraja na shule za msingi na sekondari sambamba na upatikanaji huduma za umeme na maji.

‘’Pamoja na kwamba hamnioni mara kwa mara nikija hapa Kirida kutokana na majukumu niliyo nayo lakini nimekuwa nikifanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo na haya maendeleo mnayo yaona kama vile ujenzi wa bararbara, shule, zahanati na vituo vya afya, zote ni jitihada ambazo ninazifanya’’. Alisema Mhe, Pinda.

Awali wananchi wa Kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba walimueleza mbunge wa jimbo hilo kuwa wanakabiliwa na changamoto malimbali ikiwemo kutofanyika vikao vya kijiji kwa ajili ya kujua mapato na matumizi, kuwekewa alama za mipaka maeneo ya nyumba zao kwa madai kuwa makazi hayo yapo kwenye kingo ya mto na hivyo kutakiwa kuhama wakati mto ndiyo umehama.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba wakimuangalia Bi. Adela John ambaye ni mlemavu wa miguu mara baada ya kumkabidhi baiskeli tarehe 2 Mei 2024.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda (Hayupo pichani) wakati wa mkutano wa hadahara uliofanyika kijiji cha Kirida Mei 2, 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake katika jimbo la Kavuu Mei 2, 2024.

Related Posts