Yalivyokuwa mapokezi ya katibu mkuu Umoja wa Wazazi Aly hapi kigoli Iringa

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM, Ally Hapi amewasili Mkoani Iringa kwa ajili ya kuanza ziara yake ya Mikoa minne leo May 03,2024 ambapo atakagua uhai wa Jumuiya hiyo, kufanya mikutano ya ndani na kusikiliza kero za Wananchi kwenye mikutano ya hadhara.

Hapi ameanza ziara leo May 03,2024 ambayo ataifanya hadi May 05,2024 Mkoani humo kisha ataelekea Dodoma May 07 hadi May 08,2024, Singida May 09 hadi May 11,2024 na atamalizia na Tabora May 12 hadi May 14,2024.

Hapi ambaye amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Tabora na Mara ameteuliwa hivi karibuni na kuthibitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika mabadiliko ya Sekretarieti ya CCM yaliyofanywa chini ya Mwenyekiri wa CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Related Posts