Mchezo kati ya KMC dhidi ya Kagera Sugar umemalizika Uwanja wa Azam Complex timu hizo zikiwa hazijafungana,
Licha ya mashambulizi makali ya timu zote bado safu za washambuliaji kwa timu zote hazikuweza kutikisa nyavu na kuifanya mechi hiyo kumalizika kwa suluhu hiyo.
Matokeo hayo yameongeza alama moja kwa kila timu lakini hayakubadilisha nafasi ya timu zote mbili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
KMC imeongeza alama ikifikisha pointi 33 kwenye msimamo wakati Kagera ikisalia nafasi ya saba na pointi 30.
Hiyo inakuwa sare ya pili baina ya timu hizo ambapo kwenye mchezo wa kwanza Kagera ikiwa nyumbani Novemba 22, 2023 zilifungana bao 1-1.