Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

STAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha ujio mpya wa tamthiliya ya Bridgerton, katika onesho kabambe lililowakusanya nyota daraja la kwanza kutoka Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endeela).

Onesho hilo lilifayika juzi, Mei 4, mwaka huu nchini Afrika Kusini, ambapo Netflix, waandaaji wa series hiyo, walizindua msimu wa tatu wa Bridgerton.

Msimu wa tatu wa Bridgerton unatarajiwa kurushwa na Netflix na kushuhudiwa na ulimwengu mzima  Mei 16, mwaka huu ambapo itaruka sehemu ya kwanza na sehemu ya pili  Juni 13, mwaka huu.

Katika onesho hilo, lililopewa jina la ‘Regency Era Splendor: Into The Spotlight’ lilihudhuriwa na mastaa wakubwa kutoka Kenya, Tanzania,  (Idris), Nigeria, Ghana, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini, wakiongozwa na Adjoa Andoh (ambaye amecheza kama Lady Aga kwenye Bridgerton) akiwa Kama mgeni wa heshima.

Mkali wa kurapu free style, kutoka Afrika Kusini ambaye amependekezwa kwenye Tuzo za Grammy, Musa Keys naye aliungana na mastaa wenzake katika hafla hiyo.

Mbali na Idris mastaa wengine kutoka Afrika Mashariki – Kenya walioalikwa katika onesho hilo la kijanja ni pamoja na komediani na mtayarishaji maudhui, Elsa Majimbo.

Wengine kutoka ardhi ya William Ruto ni staa wa filamu Catherine Kamau (Kate), Amina Abdi Rabar na waigizaji mahiri: Manasseh Nyagah na Jackie Matubia.

Wanamitindo maarufu wa Nairobi: Brian Babu na Lady Mandy pia walihudhuria, ambapo kwa pamoja walihusika katika kubuni na kutengeneza mavazi ya mastaa waliohudhuria.

Related Posts