Mbappe kucheza mechi yake ya mwisho akiwa na PSG mjini Paris – DW – 06.05.2024

  
Jumanne ya wiki hii utachezwa mchezo wa mkondo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya PSG na Borussia Dortmund mjini Paris, Ufaransa wakati nyota wa kalbu hiyo ambayo mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 Kylian Mbappe anatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho katika uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo Parc De Princes.

Soma zaidi. Gari la mashindano lapinduka na kuuwa watu 7 Sri Lanka

Mbappé anaondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto baada ya kuitumikia kwa misimu saba, wakitumai kuwa safari itahitimishwa kwa ushindi wa Ligi ya Mabingwa Wembley mnamo Juni 1.

PSG
Kylian Mbappe anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji katika mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa barani Uaya dhidi ya DortmundPicha: FRANCK FIFE/AFP

Lakini ili kutimiza ndoto hiyo ni sharti waifunge Borussia Dortmund ambayo tayari iko mbele kwa mguu mmoja baada ya kushinda kwa bao 1-0 katika mkondo wa kwanza nchini Ujerumani wiki iliyopita.

Mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa ambaye pia ni mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo nayo kazi ya kufanya ili kuisadia timu yake kupindua mechi hiyo hasa baada ya kushindwa kufunga katika mechi mbili za mwisho dhidi ya Dortmund.

Soma zaidi. Borussia Dortmund imeifunga Paris Saint German PSG 1-0

Kwa upande wake kocha wa PSG, Luis Enrique amesema tangu awe kocha malengo yake ni kuona kwamba wachezaji wake bora wanaisaidia timu kupata matokeo muhimu.

Campus Paris Saint-Germain
Kocha wa PSG, Luis Enrique amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza bkwa wingi katika mchezo wao dhidi ya Dortmund ili kuipa morali timu yaoPicha: Olivier Arandel/MAXPPP/dpa/picture alliance

Mbappe mwenyewe alipohojiwa na kituo kimoja cha habari nchini Ufaransa amesema anayo imani kuwa timu yake ya PSG watafanya kila linalowezekana kupata matokeo jatika mechi yao ya mkondo wa pili dhidi ya Dortmund na kupata matokeo.

Kocha Luis Enrique ana wasiwasi zaidi katika safu ya ulinzi baada ya beki wa zamani ya Bayern Munich Lucas Hernandez kupata majereha yatakayo muweka nje hadi msimu ujao.

Mshindi atacheza na Real Madrid au Bayern Munich kwenye fainali mjini London ambayo katika mchezo wa kwanza walitoka sare ya 2-2 mjini Munich.
 

Related Posts