Serikali yazidi kujiimarisha mapambano dhidi ya Ujangili

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, inaendelea kujiimarisha kwenye mapambano dhidi ya ujangili, kwa kuwajengea uwezo maafisa wake kupitia mafunzo mbalimbali pamoja na kuimarisha mahusinao mema baina ya Wizara hiyo, wadau wa Uhifadhi pamoja na wananchi kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba Jijini Dodoma alipokuwa akifungua rasmi mafunzo ya upelelezi na uendeshaji wa mashtaka kwa maafisa wa Kikosi Kazi Taifa Dhidi Ujangili kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa maafisa hao katika kukabiliana na ujangili.

CP. Wakulyamba amesema kuwa, Tanzania imejaliwa kuwa na utajiri mkubwa wa maliasili za aina mbalimbali ukilinganisha na mataifa mengine, hivyo utajiri huu unapaswa ulindwe kwa namna yeyote kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kinachokuja hivyo watu wachache wenye tabia ya ubinafsi hawatapewa nafasi ya kuhujumu maliasili hizo.

“Tanzania ina utajiri mkubwa wa maliasili ambao unapaswa kutunzwa kwa nguvu zote. Tunazo Hifadhi za Taifa 22, Mapori ya Akiba 29, Mapori Tengefu 25, Maeneo ya Ardhioevu matatu na Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori za Jamii (WMAs) 38”. Alisisitiza CP. Wakulyamba

Aidha CP. Wakulyamba aongeza kuwa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Kikosi Kitaifa Dhidi Ujangili kiliendesha operesheni mbalimbali zilizowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa na vielelezo kama vile meno mazima na vipande vya Tembo, kucha za Simba, nyamapori, Kobe hai na magamba ya Kakakuona, silaha zikiwemo za kivita na mazao ya misitu. Aidha mafanikio mengine ni kumalizika kwa kesi za wanymapori kwa watuhumiwa kutiwa hatiani.

CP. Wakulyamba ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Ujamgili huku akilishukuru shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na ujangili wa Wanyamapori na Mazao ya Misitu.

.
.
.
.

Related Posts