Watenda kazi chuo cha Mkwawa wapatiwa semina kuhusu usawa wa kijinsia katika maeneo yao ya kazi

Kaimu Rais wa chuo Kishiriki Cha Elimu Mkwawa kilichopo Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa, Profesa Deusdedit Rwehumbiza amewahimiza wafanyakazi chuoni hapo kuishi yale wanayowafundisha wanafunzi ili wanafunzi waige matendo mema kutoka kwao.

Profesa Rwehumbiza ameyasema hayo wakati wa semina kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia katika maeneo ya kazi kwa watumishi wa chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni kilimo uliopo Manispaa ya Iringa ambapo amesema ni vyema watumishi hao kuwa kioo kwani wakati mwingine wanafunzi huyafanya Yale wanayoyafanya wakufunzi wao hata pindi wanapomaliza chuo na kurejea katika jamii zao.

“Wanafunzi wanatabia ya kuiga yale tunayoyaishi sisi na kupeleka katika jamii watakapomaliza chuo, tuhakikishe tunafanya kazi zetu kwa weledi”, amesema Profesa Rwehumbiza

Katika hatua nyingine amewataka wafanyakazi hao kutumia lugha zenye staha kwa wanafunzi pia kati yao wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Lengo la kufanyika kwa semina hiyo ni kupambana na yale yatakayojitokeza katika kipindi cha utekelezaji wa mradi wa mageuzi ya uchumi ujulikanao kama (HEET) unaofadhiliwa na benki ya dunia.

Related Posts