CCM Mkoa wa Iringa yachangia Milion 5 Ujenzi wa maabara kituo cha Afya Wenda

Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Iringa wamechangia Sh Millioni tano kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya Kituo cha Afya cha St Theresia kilichopo Wenda Iringa vijijini.

Mchango huo umetolewa leo Jumanne, Mei 7, 2024 wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin aliyeambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Mkoa wa Iringa Comrade Salim Abri ( Asas) kutembelea kituo hicho.

Mchango huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa kituo hicho St Sabina Mangi.

Viongozi hao wa CCM wamemweleza St Sabina Mangi kwamba wakati wote Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi za kidini katika masuala mbalimbali, yakiwemo masuala ya huduma za kiafya.

“CCM itaendelea kuwaunga mkono ktk jitihada za kutoa huduma bora za kiafya kwa wananchi,” wamesisitiza viongozi hao wa CCM.

Akitoa shukrani kwa mchango huo, St Sabina Mangi amesema wamefarijika kutembelewa na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Mwenyekiti wa Mkoa na Mnec.

St Sabina Mengi ameshukuru sana kwa CCM kuchangia Shilingi Millioni tano kwa ajili ya ujenzi wa MAABARA ya kisasa ktk kituo hicho cha afya.

.

Related Posts