Kila mwanachama mwenye sifa anaruhusiwa kugombea nafasi yoyote,lakini kwenye uteuzi si kila mtu atateuliwa

Katibu mkuu wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa, Ally Salum Hapi amewatahadharisha watu wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi zijazo kupitia chama cha mapinduzi hususani katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani 2025 kuelewa namna mchakato wa kupata wagombea unavyokuwa kwani kwa mujibu wa katiba kila mwanachama mwenye sifa anaruhusiwa kugombea nafasi yoyote,lakini inapofika kwenye uteuzi si kila mtu atateuliwa wapo watakaoachwa ukiachwa tulia.

.

Hapi amesema hayo wakati akizungumza viongozi wa chama,jumuiya na wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma baada ya kuwasili kwa ziara ya siku tatu katika mkoa huo Hapi pamoja na kueleza malengo ya ziara hiyo lakini akatumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa wanachama wa ccm wanaojipanga kugombea nafasi za uongozi kupitia chama hicho.

.

“Hatuwezi kushinda tu uchaguzi kwa miujiza tunatakiwa kujipanga kuanzia sasa lakini pia tupate wagombe makini wanaoweza kupeperusha bendera ya ccm bila mashaka

“wapo baadhi yetu ambao hudhani kuwa lazima wateuliwa na wagombee nafasi za uongozi na wasipoteuliwa huanza nongwa na kutafuta nani mchawi,mimi nataka niwambie inapotokea hujateuliwa tulia usilete nongwa kanakwamba ilikuwa lazima uwe wewe hapana wakati wako haujafika ndiyo maana hujapata na pengine Mwenyezi mungu amekuepusha na vitu fulani kwenye hiyo nafasi kwahiyo tulia” AllyHapi

.

Related Posts