Madaktari hao ni kutoka katika Hospitali za rufaa za Amana,Temeke,Mwananyamara,Ligula na hospitali ya kanda ya kusini wanatoa huduma hizo za kibingwa kuanzia Mei 6 hadi 10,2024.
Akifungua rasmi kambi hiyo leo Mei 7,2024 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga
amesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kuhakikisha Huduma za Kibingwa na Kibingwa Bobezi zinasogezwa kwa wananchi kwaajili ya Kuwasaidi Watanzania wenye uhitaji wa Huduma hizo Katika maeneo mbalimbali.
Aidha, Ndemanga amewaomba wananchi wote wenye matatizo ya kiafya kuhudhuria katika kambi hiyo ili kuonana na kutibiwa na Madaktari Bingwa na Bingwa bobezi ambapo itasaidia kuwapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu nje ya mkoa kufuata Huduma Hizo.
Kwa mujibu wa Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine Dkt.Alexander Makala huduma zitakazotolewa kupitia kambi hiyo ni pamoja na huduma za magonjwa ya wanawake na uzazi,magonjwa ya watoto,Mifupa,Mkojo,ngozi,kinywa na meno,macho,afya ya akili,pua,koo na masikio.
Huduma zinginge ni mazoezi Tiba na viungo,upimaji wa Saratani ya mlango wa kizazi,matiti pamoja na huduma za vipimo vya maabara,mionzi na upasuaji.
Amesema huduma hizo za kibingwa zitarahisisha kwa kiasi kikubwa huduma kuwafikia wananchi na hivyo kupunguza gharama kwa wananchi kusafiri kwenda nje ya Mkoa huo kufuata huduma hizo na kwamba katika kuwafikia wananchi wengi zaidi huduma za kumuona daktari zitatolewa bure ambapo kwa wagongwa wasiokuwa na Bima za Afya watatakiwa kulipia asilimia 70 kwa huduma za vipimo, upasuaji na dawa.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya Iren Katarahiya akatumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma lukuki ikiwemo za kibingwa.
Nao bĂ adhi ya wananchi waliofika kupata matibabu hayo wakamshukuru rais samia kwa kuwasogezea huma hizo karibu yao.