Picha: Waziri wa Elimu na Viongozi wengineo walivyowasili bungeni Bajeti ya Wizara hiyo Mwaka fedha 2024/2025

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda alivyowasili Bungeni jijini Dodoma tayari kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Bajeti ya Wizara ya Elimu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ina kauli mbiu inayosema ‘Elimu ujuzi ndio mwelekeo’ ikiwa na maana msisitizo na mkazo katika mitaala yetu utajikita zaidi katika kuhakikisha wahitimu wanakuwa na ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.

.
.Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dkt. Said Mohamed akiingia Bungeni leo Mei 07, 2024 tayari kusikiliza uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
.Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu akiingia Bungeni leo Mei 07, 2024 kusikiliza uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula (kulia), Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule Ephraim Simbeye na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Sylvia Lupembe wakiingia Bungeni tayari kusikiliza uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo leo Mei 07, 2024.
.Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga akiingia katika viwanja wa Bunge tayari kwa uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo leo Mei 07, 2024.

Related Posts