80% ya Watanzania kutumia nishati Safi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema malengo ya Serikali ni kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Dkt. Biteko amesema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024 – 2034.

Amesema katika kufanikisha suala zima la utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi ya kupikia, Wizara ya Nishati itahakiisha nishati safi ya kupikia isiishie tu kwenye uzinduzi bali ilete matokeo chanya kwa wananchi. 

 

 

Related Posts