Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza leo Mei 08, 2024, wakati wa kufungua Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu y Sheria za Uchaguzi zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Balozi wa Marekani, Bw. Michael Battle akizungumza kwenye Mkutano
wa Kitaifa kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu ya sheria za Uchaguzi
zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025. katika Ukumbi wa Maktaba mpya, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).
Balozi wa Uswis Nchini, Didier Chassot, akizungumza kwenye Mkutano
wa Kitaifa kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu ya sheria za Uchaguzi
zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.katika Ukumbi wa Maktaba mpya, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe akizungumza kwenye Mkutano wa Kitaifa kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu ya sheria za Uchaguzi zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.katika Ukumbi wa Maktaba mpya, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).
Picha za pamoja.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KUELEKEA uchaguzi wa Serikali za Mtaa Oktoba, 2024 hofu ya tanda juu ya nani atasimamia Uchaguzi wa huo kati ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) au Tume huru ya Uchaguzi ambayo imeteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu y Sheria za Uchaguzi zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa hakuna dalili zozote zinazoonesha tume huru ya Uchaguzi inajiandaa kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Amesema hotuba ya bajeti ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) imeeleza kuwa inaratibu Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye vijiji 12318, mitaa 4263 na Vitongoji 64361 katika halmashauri 184 utakapfanyika 2024.
Wameshatekeleza shughuli za maandalizi ikiwa pamoja na uhakiki wa maeneo ya Utawala yatakayoshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu wa 2024.
Hivyo wameshaandaa rasimu ya tangazo la Serikali kuhusu maeneo hayo ya utawala na kuandaa rasimu ya kanuni za uchaguzi na kufanya mipango yandani ya Serikali kupata maoni ya yakujumlisha katika rasimu hiyo.
Lakini mpaka sasa Vyama vya Siasa havijashirikishwa katika maandalizi ya kanuni ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Waziri alieleza katika mwaka 2024/2025 ofisi ya Rais TAMISEMI imetenga shilingi milioni 17.8 kwaajili ya kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa serikali za Mitaa wa 2024.
Kwahiyo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utasimamiwa na TAMISEMI lakini sheria ambayo tayari imeshapitishwa inasema Jukumu la Tume Huru ya Uchaguzi ni kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Sasa Hili likoje kwamba Sheria teyari imepitishwa lakini Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utasimamiwa na TAMISEMI.
Labda wanamaelezo yanamna gani kipindi hiki cha Mpito ya TAMISEMI itashirikiana na Tume Huru ya Uchaguzi.
Awali Prof. Lipumba alisema Serikali na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekubali pendekezo la muda mrefu la wadau wa demokrasia kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na tume huru ya Uchaguzi badala ya TAMISEMI.
Licha ya hayo Prof. Lipumba aliwaomba washiriki na wadau wa demokrasia kuyajadili mambo hayo kwa kina ili kuweza kutoa mapendekezo yao.
“Nawaomba washiriki wa mkutano huu kujadiliana kwa uwazi kwa kutumia nguvu za hoja lakini pia kwa kuheshimiana kwa lengo la kujenga Taifa moja lenye mfumo imara wa kidemokrasia unaoendana na maadili ya watanzania.
Pamoja na kukosoana lakini pia hali ya kidemokrasia katika awamu ya tano ilikuwa na changamoto nzito, lakini falsafa ya 4R imetupa nguvu Mpya ya kujadili namna ya kujenga demokrasia ndani ya nchi yetu, ni mhimu tusiishie kwenye kuzungumza tuu, twende pia kwenye vitendo vya utekelezaji, Mkutano huu utafikia maazimio muafaka ambayo tutayawasilosha selikalini ili yaweze kufanyiwa kazi.” Ameeleza
Kwa Upande wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, Dkt. Mohamed Seif amekubaliana kuwa bunge lomeshapitisha sheria ya uchaguzi lakini amesema watafanya mapitio ili kuona kama kunamapungufu ili waweze kuyaweka sawa.
Amesema kuwa Mchakato ulivyokwenda wa kupitisha sheria ya chaguzi wa Serikali za Mtaa ulikwenda vizuri na walishiriki pamoja na vyama vyote vya siasa nchini lakini kama yatakuwepo mageuzi yoyote basi tutafanya mageuzi yatakayojitokeza na kuweka sheria sawa ili nchi iweze kwenda sawa.
“Tunataka nchi hii tuijenge kwa demokrasia na sisi bado tunaendeleza zile 4R za Mwenyekiti wa CCM taifa ili kuona nchi yetu inaishi kwa amani, usalama na Utulivu.”
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa haijafanyika tathmini ya kisayansi ya kujua athari za Uchaguzi wa 2019 wa serikali za Mitaa kwa kuangalia zimeathiri vipi maendeleo ya wananchi katika kijiji, Kitongoji.
Amesema kuwa hata kama kukifanyika maboresho ya sheria kiasi gani kama upande wapili hakuna utashi wa Kisiasa, Utashi wa kisheria haya mabadiliko ya kisheria yatakuwa yanapoteza muda.
Amesema kuwa mambo yaliyofanyika katika chaguzi za Serikali za Mitaa za kuanzia 20000 hadi leo 2024 Chama Chake kimekataa kufanya kutokana na kuona mambo ya zamani yanafanyika mpaka leo.