KAZI YA UREJESHAJI WA MIUNDOMBINU SOMANGA INAKAMILISHWA, NGUVU YAELEKEZWA SONGAS.

Wizara ya Ujenzi, Timu ya Wataalam kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS) ikishirikiana na Makandarasi, wanaendelea na zoezi la urejeshaji wa Miundombinu ya Barabara katika eneo la Songas ambalo nalo lilikatika katika Barabara Kuu ya Lindi – Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.

Hadi kufikia leo Mei 08, 2024 kazi ya urejeshaji wa Miundombinu ya Barabara hiyo katika eneo la Somanga ipo katika hatua za ukamilishaji ambapo magari ya mawe yamesharuhusiwa kupita kuelekea maeneo mingine yaliyoathiriwa.






Related Posts