Na Jane Edward, Arusha
Vilio, nyuso za Huzuni, Majonzi na sura zilizokufa Matumaini ni mambo yaliyotawala kwenye Nyuso za mamia ya Wakazi wa Mkoa wa Arusha waliojitokeza kwa wingi kwenye Kliniki Maalum ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda ya kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amekuwa hapa kwenye viwanja vya Ofisi yake Mkoani Arusha kuhakikisha kuwa Mawakili, watumishi wa idara mbalimbali na taasisi zinazotoa misaada ya kisheria zinawajibika kikamilifu kuwasikiliza na kutatua changamoto zote za Wananchi waliojitokeza hapa.
Makonda ameahidi kusimamia kuhakikisha kila mmoja anaridhika na maamuzi yatakayotolewa leo akiahidi pia kutoa msaada wa mawakili kwa kesi zitakazokuwa na uhitaji wa kupelekwa mahakamani.
“Leo nataka niwaambie wananchi wa Arusha hizi siku tatu ni za kwao na ninataka kila mwenye kero aje hapa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wasikilizwe na wataalamu wangu hapa kwaajili ya utatuzi”Alisema
Haya hivyo zoezi hilo limeanza leo Mei 08,2024 na likitarajiwa kukamilika Mei 10, 2024.