RAIS DK.HUSSEIN MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA MAZIKO YA MUASISI WA UWT ZANZIBAR MAREHEMU ASHA SIMBA MAKWEGA GOZA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Viongozi mbalimbali katika Sala ya Maiti ya Marehemu Asha Simba Makwega Muasisi wa UWT pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Sala hiyo iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, iliyofanyika katika Msikiti wa Maisara Wilaya ya Mjini Unguja na kuzikwa Kijijini kwao Pete Mkoa wa Kusini Unguja leo 8-5-2024.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa Wanafamilia ya Marehemu Asha Simba Makwega, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Pete Mkoa wa Kusini Unguja leo 8-5-2024.
(Picha na Ikulu)

Related Posts