Alhamisi ya TBT: Picha 15 za kitambo za Big Joe akiwa na mastaa wakubwa!!

Leo ni Alhamisi Mei 9,2024 na tunajua kwenye Ulimwengu wa leo siku hii imepewa cheo cha TBT yaani siku ya kukumbuka matukio ya zamani ambapo millardayo.com inakukumbusha au kukuonyesha picha alizowahi kupiga Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga Big Joe akiwa na mastaa mbalimbali wakubwa aliowahi kukutana nao hususani kukuza sekta ya Burudani nchini.

Pichani:Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akiwa na msanii wa Nigeria Wizkid Mwaka 2016 kwenye Tamasha la Fiesta lililofanyika Mkoani Mwanza


Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akiwa na msanii wa Marekani 50 Cent mnamo Mwaka 2008 alipokuja nchini kwaajili ya kutumbuiza

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga alipokutana na Mshambuliaji wa Zamani wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba huko USA kwenye NBA All Stars mwaka 2019.

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akimpokea msanii wa Marekani Ja Rule Airport mwaka 2006 kwaajili ya kutumbuiza nchini kwenye Tamasha la Fiesta


Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga alipokutana na Msanii wa Nigeria Banky Mwaka 2016 nchini.

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwa na Msanii wa Marekani Rick Ross Mwaka 2012 alipokuja nchini kwaajili ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Fiesta.

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwa na msanii wa Marekani Busta Rhymes Mwaka 2009 alipokuja nchini kwaajili ya kutumbuiza katika Viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Group Joseph Kusaga akiwa na Mwanamuziki kutoka Jamaica, Orville Richard Burrell ‘ Shaggy’ mwaka 2008 alipokuja nchini kwaajili ya kutumbuiza Kwenye Tamasha la Fiesta.

Pichani: Wasanii kutoka Marekani Beyoncé na Jay Z walipofika nchini mnamo 2009 walizindua mradi wa huduma ya maji kwenye eneo la Mwananyamala Jijini Dar es Salaam

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Group Joseph Kusaga akiwa na Msanii wa Marekani Eve Alipowasili nchini

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Group Joseph Kusaga akiwa na msanii wa Marekani Ludacris mwaka 2011 alipokuja kwenye Tamasha la Fiesta..

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Group Joseph Kusaga akiwa na msanii Oliver Mtukudzi Mwaka 2016…

Pichani: Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwa na wakali Morgan Heritage

Related Posts