Bacca: Mama yangu anamkubali Job

BEKI kisiki wa Yanga, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ amesema mama yake ambaye ni shabiki mkubwa wa Simba, anavutiwa na aina ya uchezaji wa beki wa kati na nahodha msaidizi wa Yanga, Dickson Job.

Bacca alisema hayo jana baada ya kutamatika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao Yanga iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar mfungaji akiwa Mudathir Yahya dakika ya 82.

Beki huyo wa zamani wa KMKM alisema Job ni mchezaji anayejitoa uwanjani na kwa kushirikiana pamoja wametengeneza ukuta imara ndani ya kikosi cha Yanga.

“Kwakweli Job ni mtu anayejitoa sana, kila mtu anaona nadhani mama yangu mzazi amewahi kumzungumzia sana akisema ni mchezaji anayemvutia sana,” alisema Bacca.

Yanga imefikisha pointi 68 katika michezo 26 iliyocheza hivyo ikihitaji pointi tano tu ili kufikisha 73 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ambazo zitaipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo.

Kwenye mechi 10 za mwisho ilizocheza Yanga msimu huu mabeki hao wawili Job na Bacca wameruhusu bao moja tu dhidi ya Simba Aprili 20, mwaka huu huku wakiambulia clean sheet tisa.
Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns
Mamelodi Sundowns 0-0 Yanga
Dodoma Jiji 0-2 Yanga
Singida Fountain Gate 0-3 Yanga
Yanga 2-1 Simba SC
JKT Tanzania 0-0 Yanga
Yanga 1-0 Coastal Union
Yanga 3-0 Tabora United
Mashujaa FC 0-1 Yanga
Yanga 1-0 Kagera Sugar

Related Posts