Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Ilala kukagua miradi 7 yenye thamani ya Tsh Bil.40

Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam umekimbizwa umbali wa KM 81.7 na kupitia miradi 7 yenye thamani ya Tsh 40,941,764,931

Mwenge wa Uhuru katika Wilaya hiyo ukiongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg Godfrey Eliakimu Mnzava umetembelea, umekagua, umeweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo.

Aidha miradi ambayo imepitiwa na Mwenge huo ni Ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo 45 Shule ya Sekondari Minazi mirefu, Kituo cha Polisi Mwanagati, Kituo cha Afya Kinyerezi, Kituo cha kutengeneza mapambo ya Gypsum Good Hope Segerea, Barabara ya Tukuyu Km 0.62 kwa kiwango cha lami, na mradi wa utoaji elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Alimuntazir.

Miradi yote iliyopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ilala imepitishwa na Mwange huo hakuna mradi uliokataliwa

Sanjari na hilo katika maeneo yote ambayo Mwenge wa Uhuru umepita umeendelea kuelimisha Wananchi juu ya Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe pamoja na Rushwa.

Related Posts