RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MALORI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Profesa Kitila Mkumbo mara baada ya kuzindua Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam

…….

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kujenga uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi.

Aidha, Rais Samia amesema sekta ya viwanda inaongeza uzalishaji na kutoa ajira kwa wananchi, jambo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi jumuishi na kusaidia katika mapambano ya kuondoa umasikini.  

Rais Samia amesema hayo leo wakati akizindua kiwanda cha kuunganisha malori na matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo wilaya ya Kigamboni.

Rais Samia pia amesema serikali imepunguza kodi ya makampuni kutoka 30% hadi 10% kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo ili kuchochea uwekezaji zaidi kwenye sekta ya viwanda. 

Vile vile, Rais Samia amesema kiwanda hiki ni chachu ya ukuaji wa viwanda na sekta nyingine kwa kuwa kinatumia vioo vinavyozalishwa na kiwanda kingine, ambacho zaidi ya 80% ya malighafi zake pia zinapatikana hapa nchini. 

Hivyo, matumizi ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini yanapunguza gharama kwa kampuni yenyewe inayotengeneza magari na pia inaongeza manufaa ya uwepo wa kampuni hiyo kwa uchumi wa nchi. 

Kiwanda hiki kitatoa ajira za moja kwa moja takribani 250 na zisizo za moja kwa moja 1,800, kuongeza mzunguko wa fedha, mapato ya serikali na kuhaulisha teknolojia.  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya mojawapo ya Gari lililounganishwa katika Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Watumishi wa Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam mara baada ya uzinduzi tarehe 09 Mei, 2024. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watumishi wa Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited mara baada ya uzinduzi uliofanyika Kiwandani hapo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited Bw. Chetan Chug wakati akikata utepe kuzindua Kiwanda hicho kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuzindua Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Profesa Kitila Mkumbo mara baada ya kuzindua Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited Chirag Panna wakati akikagua kazi mbalimbali za kuunganisha magari kiwandani hapo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Kiwanda cha Saturn Corporation Limited Bw. Chetan Chug pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Chirag Panna mara baada ya kukagua shughuli mbalimbali Kiwandani hapo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.
[5/9, 2:06 PM] Sharifa Ikulu: Taswira ya magari mbalimbali yaliyounganishwa katika Kiwanda cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.
    Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

  

Taswira ya Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited mara baada ya uzinduzi uliofanyika Kiwandani hapo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

Related Posts