Rais Samia azindua Kiwanda cha kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited Kigamboni Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited Bw. Chetan Chug wakati akikata utepe kuzindua Kiwanda hicho kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuzindua Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Profesa Kitila Mkumbo mara baada ya kuzindua Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited Chirag Panna wakati akikagua kazi mbalimbali za kuunganisha magari kiwandani hapo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Kiwanda cha Saturn Corporation Limited Bw. Chetan Chug pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Chirag Panna mara baada ya kukagua shughuli mbalimbali Kiwandani hapo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

Taswira ya magari mbalimbali yaliyounganishwa katika Kiwanda cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

Related Posts