Ubaguzi wa rangi unachangia umaskini Ujerumani – DW – 09.05.2024

Watu weusi, waislamu na Waasia wanaoishi nchini Ujerumaniwamo katika wasiwasi mkubwa wa kutumbukia katika umasikini licha ya elimu nzuri. Ubaguzi wa rangi umeenea sana nchini Ujerumani. Jee hii inamaanisha nini kwa wale wanaoathirika?

Kituo cha Ujerumani cha Utafiti wa Ushirikiano na Uhamiaji cha mjini Berlin kilichapisha utafiti juu ya “Mipaka ya Usawa. Katika ripoti yao watafiti wa chuo hicho wanabainisha mwambato uliopo kati ya ubaguzi wa rangi na hatari ya umaskini.

Ujerumani yaruhusu matumuzi ya bangi

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Watafiti wa masuala ya kijamii Zerrin Salikutluk na Klara Podkowik wamefanya uchunguzi wao kwa kutumia msingi wa taarifa za kituo cha kitaifa kinachofuatilia masuala ya ubaguzi wa rangi nchini Ujerumani.

Katika uchunguzi wao wamebainisha ubaguzi katika mfumo wa elimu, katika sekta za uajiri, nyumba na pia katika sekta ya afya. Chunguzi za hapo awali pia zimeonesha kwamba watu wenye nasaba ya uhamiaji wanabaguliwa inapohusu fursa za  ajira. Hali hiyo inaongeza uwezekano wa watu hao kuishi katika umasikini.

Soma: Ujerumani inataka kupunguza mafao ya wakimbizi?

Hapa nchini Ujerumani mtu anahesabika kuwamo katika hatari ya kuishi katika umasikini ikiwa kipato chake kipo chini ya asilimia 60 ya pato la wastani yaani Euro 1310. Asilimia 5 ya wazawa wanaofanya kazi kikamilifu, wamesema mapato yao yamepungua hadi kufikia chini ya pato hilo la wastani.

Lakini kwa watu wenye nasaba ya uhamiaji idadi yao imeongozeka hadi asilimia 20. Hayo yanhujsu pia kwa wahamiaji wenye elimu ya viwango vya juu. Watu wanaobaguliwa wamo katika hatari ya kukabiliwa na hali ngumu za maisha, mara saba zaidi ya wanajamii wengine, hapa nchini Ujerumani.

Je, uhamiaji ni tishio kwa Ujerumani?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Idadi kubwa ya wahamiaji walioingia nchini Ujerumani kuanzia mwaka wa 2013 hasa ndiyo wanaokabiliwa na hatari kubwa ya kutumbukia katika umasikini. Watu hao hasa wametokea Syria na Afghanistan nchi  ambazo zilipitia misukosuko ya vita. Watu hao wamo katika uwezekano mkubwa wa kukumbwa na umasikini kutokana na kuwapo kwa fursa finyu kwao, za kupata ajira za maana.

Soma: Kuzorota uchumi wa Ujerumani ni changamoto kwa Ulaya ya kati

Mtafiti Salikutluk amesema pia watu wenye nasaba nyingine ambao wameishi nchini Ujerumani kwa muda wa miaka mingi au waliozaliwa hapa nchini nao pia wamo mashakani. Watu hao pia wanabaguliwa licha ya kuwa na uraia wa Ujerumani.

Ushahidi ulipatikana baada kuomba kazi kwa kutumia majina mawili tofauti. Matokeo yake ni kwamba aliyetuma barua  ya  kuomba kazi kwa kutumia jina la kituruki hakuwa na matumaini makubwa ya kuitwa kwa ajili ya kujitambulisha kwa mwajiri.

Yuro
Pesa ya Ulaya ya yuroPicha: K. Schmitt/Fotostand/picture alliance

Mtafiti huyo, Salikutluk anaamini kwamba uchunguzi uliofanywa unaweza kusaidia katika juhudi za kupambana na  umasikini na wakati huo huo kuhimiza haja ya kuwepo fursa sawa kwa wote.

Watafiti hao wanasema pana haja ya kutambua elimu ambayo wahamiaji wamepata katika nchi zao za uzawa. Wamesema ni kwa njia hiyo tu kwamba wahamiaji watawezeshwa kuingia katika soko la ajira katika msingi wa haki sawa. Watu hao wataweza pia kufanya kazi za waajiriwa wenye ustadi.

Soma pia: Nusu ya makampuni ya Ujerumani yakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi

Ili kuweza kuuharakisha mchakato wa kuleta utangamano kwenye soko la ajira wataalamu wametoa wito wa kuwawezsha watu wenye nasaba za uhamiaji kupata ustadi wa lugha ya kijerumani.

Watafiti hao wamesema kiwango cha juu cha umasikini miongoni mwa wahamiaji kinaweza kupunguzwa na kuondoshwa ikiwa watu hao watapata fursa za ajira. 

 

Related Posts