WAZIRI AWESO ABAINISHA MIRADI YA MAJI ILIYOKAMILIKA NA INAYOENDELEA


“Wizara ya Maji imekamilisha miradi mikubwa na ya kimkakati ikiwemo mradi wa maji Arusha ambao umeongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 40 hadi lita milioni 200 kwa siku na muda wa upatikanaji wa huduma ya maji kutoka saa 12 hadi saa 24 kwa siku.”

“Pia , mradi wa maji wa Butimba unaonufaisha wakazi wapatao 450,000 katika Jiji la Mwanza umekamilika na wanachi wanapata maji safi na salama”

“Aidha, Mradi wa ujenzi na uboreshaji wa mtandao wa majisafi Nzuguni (Awamu ya kwanza) umekamilika na unanufaisha wakazi 75,968.”

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji Nchini Mhe. Jumaa Aweso wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 Bungeni Jijjini Dodoma, leo tarehe 9 Mei, 2024.

#UwasilishajiWaMakadirioYaBajeti

#WizaraYaMaji2024/2025

#KaziIendelee


Related Posts