RC Malima ataka wanahabari Morogoro kuwa mabalozi wa Utalii

Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amewataka wanahabari mkoani humo kuwa mabalozi wa utalii Kwa kuandika Habari na makala mbalimbali zitakazowavutia watalii wengi kutoka nje na ndani ya nchi.

RC Malima ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo kwa wanahabari zaidi ya 30 yaliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa habari Tanzania (TAMPA) kwa kushirikiana na TANAPA akisema Mkoa wa Morogoro unahifadhi Tatu Kubwa ambazo ni Mikumi,Udzungwa na Mwalimu Nyerere ambazo zinatosha kuwa namba moja kwemye sekta hiyo.

RC Malima amesema bado hamasa ni dogo Kwa wanahabari Kuhusu uandishi wa Habari za utalii na Mazingira hivyo akaahidi kugharamia wanahabari waliohudhiria mafunzo hayo kuzunguka katika hifadhi hizo kuona vivutio vilivyopo na kuvitangaza.

“Nataka timu ya Waandishi wa Habari 40 tukafanye utalii , tulale Mikumi kisha twende Udzungwa na badae Mto Kilombero tukitoka hapo nataka Morogoro iwe namba moja Kwa utalii nchini”

Aidha Malima amesema serikali ina mpango kufungua geti lingine kupitia Kilosa kuingia Hifadhi ya Taifa ya mikumi kutokana na kuwepo Kwa treni ya mwendokasi Ili kurahisisha shughuli za utalii katika hifadhi hiyo ambapo kwa Sasa wanalazimika kusafiri zaidi ya kilometa 100 kutoka kilosa Hadi Mikumi na endapo geti Hilo litafunguliwa watasafiri kilometa 15 kuingia hifadhini.

Anasema hifadhi ya Mikumi inafikika kwa urahisi kwa kutumia njia mbalimbali ambazo ni barabara ya TAZAM, Reli ya kati na Reli ya SGR na njia ya anga hivyo watalii wanapata fursa ya kuona wanyama kirahisi.

Pamoja na hayo amewataka wadau mbalimbali kuanza kujenga hoteli nzuri zenye viwango katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kisaki Ili kuhudumia watalii wanaotembelea hifadhi ya Mwalimu Nyerere, Mikumi, Doma Kwa hifadhi ya Mikumi na Ruaha kwa hifadhi ya Udzungwa.

Kwa Upande wake Rais wa TAMPA, Simon Mkina amesema lengo la semina hiyo ni kuwaandaa wanabari kuwa sehemu ya utalii Kwa kushiriki moja kwa moja Ili kutimiza malengo ya Serikali kupitia filamu ya THE ROYAL TOUR.

“Tumeanzia Dar es Salam na leo tupo Morogoro tunatoa mafunzo haya Kwa kushirikiana na wakufunzi kutoka Chuo Cha Taifa cha Utalii Ili kupata mabalozi wazuri masula ya utalii na watalii

Naye Mkufunzi Mwanadamizi Chuo cha Taifa cha Utalii Agapiti Roman amesena mwaka 2023 jumla ya watalii Milioni 1.8 walitembelea Hifadhi za Taifa nchini kutoka Mili. 1.3 mwaka 2022 na hii ni niongezeko kubwa baada ya filamu ya THE ROYAL TOUR ambayo imekua chahu kubwa kwa nchi.

Naye katibu wa chama wa Waandishi wa Habari mkoa Morogoro (MORO PC) Lilian Kasenene ameshukuru kwa niaba ya waandishi wa habari Morogoro Kwa kupata mafunzo hayo ambayo yamewajenga wanahabari kuwa na utayari wa kuripoti masuala ya utalii.

Related Posts