Ouma anavyoibeba Coastal Union Ligi Kuu

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, David Ouma amefanikiwa zaidi kutengeneza timu kimbinu na kiufundi, akijitahidi kumfanya kila mchezaji kuwa bora katika nafasi yake.

Kocha huyo ambaye alianza kuifundisha Coastal Union, Novemba 9, mwaka jana akichukua mikoba ya Mwinyi Zahera ambaye alishindwa kuendana na kasi ya timu hiyo tayari ameanza kuandika rekodi zake ndani ya kikosi hicho.

Ouma amevuja uteja kwa timu hiyo kumaliza msimu ikiwa na pointi chache kwani misimu mitatu nyuma ilimaliza na pointi 33, 38, na 40 ambazo inaweza kuzifikia na zaidi endapo itapata ushindi katika michezo iliyosalia.

Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania waliobeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara (enzi za Ligi Daraja la Kwanza) mwaka 1988, juzi ilipata ushindi nyumbani dhidi ya Singida Fountain Gate kwa kuifunga mabao 2-0 na kuendelea kujikita katika nafasi ya nne ikifikisha pointi 37 katika mechi 26 na kusaliwa na michezo minane.

Ouma ambaye alichukua mikoba ya Zahera amefanikiwa kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye msimamo ameshinda mechi tano mfululizo kwenye mechi zake 17 ambazo ameiongoza timu hiyo tangu amekabidhiwa.

Kocha huyo ametengeneza rekodi yake ndani ya Coastal Union baada ya miaka mingi na inaonyesha anaweza kuwatesa wenzake kwa muda mrefu, kwani amedhihirisha ushindani ni namna ya kutumia mbinu tofauti dhidi ya wapinzani.

Hakuna ambaye aliiweka Coastal Union kwenye mbio ya kuwania nafasi nne za juu huku wengi wakiipa Singida Fountain Gate kutokana na kuwa mastaa wengi wa kigeni na ndio timu ambayo ilipata nafasi hiyo msimu uliopita, lakini mambo yamekuwa tofauti msimu huu.

Katika michezo 26 ambayo Coastal Union imecheza imeshinda 10, sare saba na kufungwa tisa na Ouma ameiongoza kwenye mechi 17 akishinda tisa, sare tatu na kufungwa mitano.

Mechi za ushindi ni dhidi ya Tanzania Prisons Novemba 23 (1-0), Geita Gold (3-0), Kagera Sugar (0-1), JKT Tanzania (0-1), Dodoma Jiji (0-1), Mtibwa Sugar (0-1), Ihefu FC (0-1),Mashujaa (1-2) na Singida Fountain Gate (0-2).

Vipigo ilivyopata Coastal Union chini yake ni dhidi ya Singida Fountain Gate mchezo wa kwanza mabao 2-1, Tabora United 1-0, Simba 2-1, Namungo 1-0 na Yanga bao 1-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ouma alisema anajivunia kuinoa Coastal Union alikokutana na wachezaji wenye uchu wa mafanikio na wamekuwa wakifanya kile anachowaelekeza ili wafikie lengo walilojiwekea mwishoni mwa msimu.

“Nimekuta malengo ya kumaliza nafasi tano za juu. Nafurahi nakimbizana na malengo kutokana na mchango mzuri wa wachezaji kuendana na mbinu zangu. Bado tuna kazi ya kufanya kuhakikisha tunafikia malengo hayo,” alisema.

Novemba 23, Coastal Union vTZ Prisons                (1-0)

Novemba 27, Singida FG    vCoastal          (2-1)

Novemba 30, Coastal Union vGeita Gold               (3-0)

Desemba 12 Coastal Union  vKagera Sugar (1-0)

Desemba 18 JKT Tanzania   vCoastal Union(0-1)

Februari 12 KMC           vCoastal Union(0-0)

Februari 15 Coastal Union vDodoma Jiji  (1-0)

Februari 24 Coastal       vMtibwa Sugar (1-0)

Machi 3 Tabora United     vCoastal Union(1-0)

Machi 6 Azam FC                vCoastal Union(1-1)

Machi 9 Simba                     vCoastal Union(2-1)

Machi 14, Coastal Union   vIhefu               (1-0)

April 12, Mashujaa             vCoastal Union(1-2)

April 17, Namungo             vCoastal Union(1-0)

April 27, Yanga     vCoastal Union(1-0)

Mei 6, Coastal Union        vTZ Prisons       (0-0)

Mei 10, Coastal Union      vSingida FG   (2-0)

Related Posts