Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Dk. Biteko ametoa kauli hiyo leo Jumamosi jijini Dodoma katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Chama hicho alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Viongozi, wadau na wananchi wakiwa katika hafla ya maadhimisho ya Miaka 62 ya Chama Cha Msalaba Mwekundi Tanzania iliyofanyika leo tarehe 11 Mei 2024 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Dk. Biteko. Aidha, maadhimisho hayo yamehudhuriwa na washiriki kutoka nchi za Uganda, Spain, Botswana, Kenya, Ubeligiji na Qatar.