WAZIRI MKUU AKAGUA SHAMBA LA MKULIMA WA KAKAO, KYELA

Waziri Mkuu Kasssim Majaliwa leo Mei 12, 2024 ametembelea shamba la Mkulima zao la Kakao Clement Msalangi lililopo kijiji cha Mababu, Wilayani Kyela Mei 12,

Akizungumza baada ya kulitembelea Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakulima wa zao hilo wajisajili na watambue idadi ya miche waliyonayo na ukubwa wa mashamba yao ili wakati Serikali ikitoa ruzuku kila mkulima anufaike na kuiwezesha Serikali kujua ni tani kiasi gani itazalishwa.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wakulima na viongozi wa AMCOS wasimamie ubora zao la Kakao na kuzitumia fedha wanazopata baada ya mauzo kujiletea maendeleo katika maeneo yao.







Related Posts