Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetambulisha rasmi huduma
yake ya kidigitali ya ‘NBC Connect’ Visiwani Zanzibar. Huduma hiyo ya kisasa
mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali huwezesha huduma salama na
haraka za kibenki kwa njia ya mtandao ikiwa ni muitikio wa benki hiyo katika
kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ujumuifu katika huduma za kifedha
(financial inclusion).
Hafla ya utambulisho wa huduma hiyo ilifanyika mwishoni
mwa wiki Zanzibar ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji. Hafla hiyo pia ilihusisha uwepo wa wateja wa benki
hiyo visiwani humo, huku wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja
wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya.
Akizungumza kwenye tukio hilo lilidumu kwa siku tatu ambalo
ni muendelezo kufuatia matukio kama hayo yaliyofanyika mikoa ya Kanda ya Nyanda
za Juu Kusini na Kanda ya Ziwa, Kapya alisema huduma hiyo ya kidigitali ni
uthibitisho wa dhamira ya benki hiyo kuwapatia wateja wake huduma bora za
kibenki ambazo ni rahisi, salama na zinazofaa na kukidhi mahitaji ya wateja.
“Kinachofanyika leo ni utambulisho rasmi wa huduma hii
kwa kuwa tayari wateja wetu wameshaipokea huduma hii na wanaifurahia. Tupo hapa
kupata mrejesho na kutoa ufafanuzi kwenye maeneo muhimu ili waweze kuifurahia
huduma hii kwa upana wake. Ikitumika vizuri huduma hii, wateja wetu wenye
makampuni na taasisi mbalimbali zilizopo visiwani Zanzibar watapata fursa na
uwezo wa kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu mpya
katika kupata huduma za kibenki.’’ Alisema.
Akiizungumzia huduma hiyo, Dkt. Mngereza alisema
imesaidia kuleta mapinduzi mapya katika utoaji wa huduma za kibenki huku
ikichochea kasi ya ukuaji uchumi kupitia urahishwaji wa malipo na ukusanyaji wa
mapato mbalimbali yakiwemo ya serikali.
“Utambulisho wa huduma hii ya NBC Connect hapa
Zanzibar unakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
katika kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia huduma bora za kifedha na
uchumi jumuishi. Kupitia huduma hii mashirika na taasisi mbalimbali zitaweza
kufanya malipo kwa wakati bila usumbufu na kwa kuwa ni rahisi kwa huduma hii
kuwafikia walengwa kwa wingi wao basi pia
itachagia ukuaji wa uchumi…naomba sana mashirika, taasisi na kampuni
mbalimbali hapa Zanzibar waipokee huduma hii,’’ alisema
Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo Mkuu wa Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC, Bw
Jimmy Myalize alisema huduma hiyo inawapa wateja uwezo wa kufanya miamala
kirahisi popote, wakati wowote ikiwemo kufanya malipo ya ndani na nje ya nchi,
malipo ya serikali pamoja na malipo kwa mkupuo bila kutumia muda mrefu kwa
kutumia tu simu au kompyuta.
“Wateja pia wataweza kupata taarifa za miamala
waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki. Huduma hii imetengenezwa
kwa teknalojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezingatia na
kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo
huakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.’’ Aliongeza.
Aliongeza kuwa pamoja na huduma hiyo benki hiyo imejipanga
kutoa usaidizi binafsi kwa wateja kupitia kituo chake cha huduma kwa wateja
ambapo wataalamu wa huduma hiyo wamejipanga kuwasaidia wateja kulingana na
mahitaji yao na kutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia jukwaa hilo kwa ufanisi.
Meneja wa Huduma za Miamala wa Benki ya NBC Charles Ndendeje akifafanua kuhusu huduma
ya kidigitali ya ‘NBC Connect’ inayotolewa
na benki hiyo mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma
hiyo kwa wateja wa benki ya NBC Zanzibar iliyofanyika mwishoni mwa wiki
Zanzibar. Hafla hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji (wa pili kushoto) akijadili jambo na maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakati wa hafla
fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’ inayotolewa na benki hiyo mahususi kwa
makampuni pamoja na taasisi mbalimbali iliyofanyika
mwishoni mwa wiki Zanzibar. Kushoto ni Mkuu
wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya,
Meneja wa Benki hiyo tawi la Zanzibar Ramadhan Lesso (wa pili kulia) na Mkuu wa
Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC, Jimmy Myalize (Kulia)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji (pichani) akizungumza na wageni
waalikwa wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC
Connect’ inayotolewa na benki ya NBC mahususi
kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali
iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa
serikali Benki ya NBC Linley Kapya (pichani) akizungumza na wageni waalikwa
wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC
Connect’ inayotolewa na benki ya NBC
mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Zanzibar Ramadhan Lesso
(Pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa
huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’
inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi
mbalimbali iliyofanyika mwishoni mwa
wiki Zanzibar.
Mkuu wa Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC,
Jimmy Myalize (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya
utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’ inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa
makampuni pamoja na taasisi mbalimbali
iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC pamoja na maofisa wa
benki hiyo wakifuatilia utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC
Connect’ inayotolewa na benki ya NBC
mahususi kwa makampuni pamoja na taasisi mbalimbali ulofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji (katikati -walioketi) akiwa kwenye
picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya NBC wakati wa hafla
fupi ya utambulisho wa huduma ya kidigitali ya ‘NBC Connect’ inayotolewa na benki ya NBC mahususi kwa
makampuni pamoja na taasisi mbalimbali
iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.