Kiwango cha biashara baina ya Tanzania na Uganda chafikia Dola Millioni 400

Kiwango cha biashara baina ya Tanzania na Uganda kina kadiriwa kufikia thamani ya dola za marekani milioni 400 mpaka disemba mwaka jana ambapo Tanzania imeuza bidhaa na huduma nchini Uganda zenye thamani ya dola milioni 196 ikilinganishwa na dola milioni 186 za mauzo ya bidhaa na huduma nchini kutoka Uganda.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mtendaji wa TIC Gilead Teri wakati akizungumzia mkutano wa kibiashara baina ya Tanzania na Uganda ambapo amesema .


“Fursa ni pana na zinazoangaliwa ni sekta za viwanda,kilimo,ufugaji lakini pia tunategemea sekta ya Utalii na huduma za kifedha na wale wenzetu wa sekta ya madini, mafuta na gesi pia wenywe kutakuwa na fursa za kushiriki kwenye kongamano hilo.”

Pia aliongeza kwa kusema kuwa wanategemea kupata wadau wengi wa private sekta lakini pia TIC kama taasisi ya sekta binafsi inawatia hamasa wageni kuja nchini na kufanya kazi kwa kushirikiana kati ya Tanzania na Uganda.

Related Posts