SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAIPONGEZA KAMPUNI YA GLOBAL EDUCATION LINK

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Ali Abdulgulam Hussein akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea katika tawi la Global Education Link Zanzibar.

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Ali Abdulgulam Hussein katika time akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Zanzibar Bi Aida Maulidi Juma wakatii walipotembelea latika tawi la Global Education Link, kushoto ni Adumalk Mollel Mkurugenzi Mtendaji Global Education link kulia.

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeipongeza Kampuni ya Grobal Education Link kwa kutoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu katika kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kusoma nje ya Nchi na kuleta tija kwa Taifa.

Akizungumza leo Mei 13, 2024 wakati alipofanya ziara ya kutembelea ofisi ya Groba Education Link tawi la Zanzibar, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amani Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hassein, amesema kuwa Wizara inaendelea kufanya kazi ya mawakala wa vyuo vya elimu ya juu waaminifu.

Mhe. Hassein amesema kuwa kuna changamoto ya baadhi ya mawakala ambao sio waaminifu na kuwadanganya vijana jambo ambalo limeleta usumbufu kwa wazazi Zanzibar.

“Nitafanya ziara ya kukagua mawakala wote wa vyuo vya elimu ya juu ili kubaini ambao wanafanya kazi hii bila kuwa na kibali na kuwafungia wote watakaobainika wanafanya kazi kinyume na utaratibu” Mhe. Hassein.

Amesema kuwa Wizara ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Grobal Link Education, huku akisisitiza uongozi wa kampuni hiyo kuwasilisha mapendekezo rasmi ya kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kwa ajili ya kuanza programu ya kuwasomesha wanafunzi nje ya nchi.

Mhe. Hassein amesema kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ameifanya sekta ya elimu kuwa kipaombele katika serikali yake kwa kusomesha vijana hasa baadhi ya fani ambazo zinawataalamu wachache.

Amefafanua kuwa wamepoteza wataalamu wengi kutokana hakuna vyuo vya kutosha, hivyo serikali imeongeza bajeti katika Wizara ya elimu kwa ajili ya kusomesha wanafunzi.

Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Grobal Education Link Bw. Abdulmalik Mollel, amesema kuwa ni muhimu kuzalisha rasilimali watu wenye uweledi ambao watafanya kazi kwa ufanisi kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi.

Bw. Mollel amesema kuwa wakati umefika wa kuangalia namna ya kuzalisha vijana ambao wanaweza kutumika katika kuhakikisha Taifa linapiga hatua katika maendeleo.

“Leo vijana wengi wanamaliza kusoma alafu wanalalamika hawana ajira, jibu linakuja hawajaandaliwa katika elimu ya dunia, sisi tunaangaika kutafuta ajira lakini kuna baadhi ya nchi wanatafuta wafanyakazi” amesema Bw. Mollel.

Amesema kuwa wakati wa kutumia elimu katika kufanikisha maendeleo ikiwemo kutangaza utalii kwa kutumia wanafunzi wa elimu ya juu ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika utendaji kazi.

Related Posts