Watu saba wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa kwenye ajali mkoani Morogoro

Watu saba wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya kutokea ajali iyohusisha gari aina Noah yenye namba za usajili T.101 DKB ikitokea Dumila kuelekea Morogoro mjini kugongana uso Kwa uso lori la Mizigo lenye namba za usajili RAS 980 XV likitokea Morogoro kuelekea Dodoma

Ajali hiyo imetokea majira ya saa Mbili asubuhi eneo la Dakawa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro barabara kuu ya Morogoro -Dodoma

Mganga mfawidhi hospital ya Wilaya Mvomero Dokta Frances Paul amethibitisha kutokea kwa Vifo ambapo majeruhi mmoja amepewa Rufaa kupelekwa hospital ya mkoa Morogoro wengine sita wanaedelea na matibabu

RPC Mkoa Morogoro SACP. Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema marehemu na majeruhi Wote wametoka kwenye Noah huku chanzo cha ajali uzembe dereva Lori kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari ambapo dereva wa Lori anatafutwa Kwa kusababisha ajali hiyo .

 

Related Posts