27 wa tuma kwa namba hii wanashikiliwa na jeshi la polisi Dar es salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam inawashikilia watu 27 kwa tuhuma za utapeli kupitia mtandao huku likikamata simu zaidi ya 41 na laini 88 za simu ambazo zinadaiwa kutumika kutuma jumbe za ulaghai wa utapeli wa fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ikiwemo jijini Dar es salaam

Akizungumza leo jijini Dare es salaam laam kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao ni kutoka sumbawanga,ifakara na Rukwa ambapo wamekamatwa kufuatia oparesheni inayo endelea kwa kushirikiana na mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA .

Aidha muliro amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao 27 wanafanya jumla ya watuhumiwa waliokamatwa na kushtakiwa kufikia 83 ndani ya muda mfupi huku akiwasihi wananchi kuacha tamaa ya pesa za haraka kupitia jumbe za ulaghai zinazotumwa katika simu zao.

Watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa na jeshi la.pilisi wqkato mchakato wa kuwapeleka mahakani ukiwa unaendelea

Related Posts