UONGOZI wa Azam FC, umemuongeza mkataba beki wa kulia, Nathaniel Chilambo ambaye ataendelea kubaki katika viunga vya Azam Complex hadi 2026.
Chilambo alijiunga na Azam FC, Julai 6, 2022 akitokea Ruvu Shooting ambayo sasa inashiriki Championship baada ya kushuka Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa mtandao wa kijamii ‘Instagram’ wa timu hiyo umethibitisha kumuongeza mkataba wa miaka miwili beki huyo.
Chilambo ambaye amekuwa bora eneo la ulinzi anaungana na Pascal Msindo ambaye pia ameongezwa mkataba akiendelea kuitumikia hadi 2027.
Wachezaji hao wote wanacheza beki, Msindo akicheza kushoto huku Chilambo akicheza kulia.