Dkt.Biteko ateta na balozi wa Marekani nchini

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Michael Battle Sr. kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwamo matumizi ya vyanzo mbalimbali vya nishati ya umeme

Mazungumzo hayo yamefanyika Mei 14, 2024 katika Ofisi ndogo za Wizara, Jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya umeme ikiwemo upepo, jotoardhi, jua na gesi asilia ikiwa njia mojawapo ya kuchagiza maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Dkt. Biteko amesema kuwa mahitaji ya nishati ya umeme nchini yamekuwa ya kiongezeka kwa kasi kufuatia ukuaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ya kijamii.

Related Posts