Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana yajivunia maendeleo

 

AFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)Nicodemus Mkama amesema kitendo cha kuorodheshwa kwa hatifungani ya Kijani ya kuboresha miundombinu ya maji na utunzaji wa mazingira Tanga, kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ni hatua kubwa sana kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Mei 2024 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa hati fungani ya kijani ya kuboresha miundombinu ya Maji na utunzaji wa Mazingira Tanga kwenye soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).

Amesema kuwa hiyo ni hatua muhimu katika maendeleo na ustawi wa sekta ya fedha na uchumi hapa nchini na Afrika kwa ujumla.

Pamoja na kukusema kuna hatua muhimu katika maendeleo na ustawi wa sekta ya uchumi hapa nchini na Afrika kwa ujumla pia ametaja majukumu muhimu ya CMSA.

Ameyataja majukumu ya Mamlaka hiyo kwa kueleza kuwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ina jukumu la kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba shughuli katika masoko ya mitaji zinafanyika kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili kuleta uwazi na haki kwa washiriki wote.

Amesema kuwa Masoko ya mitaji ni sehemu ya mfumo wa sekta ya fedha inayowezesha upatikanaji wa fedha za muda mrefu, yaani zaidi ya mwaka mmoja, kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo.

“Fedha za kugharamia shughuli za maendeleo hupatikana kwa kuuza hisa za kampuni (shares), hatifungani za kampuni (corporate bonds), hatifungani za taasisi (Subnational Bonds), hatifungani za Serikali (Government bonds) na vipande katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Schemes).

“Fedha hupatikana kutoka kwa wawekezaji, ambao ni watu binafsi, taasisi na kampuni na hatimaye fedha hizo huwekezwa katika sekta za uzalishaji na hivyo kuchochea ustawi na maendeleo ya uchumi”ameeleza Mkama.

“Katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi madhubuti wa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisaidiwa na Waziri wa Fedha kuisimamia Sekta ya Fedha, Masoko ya Mitaji Tanzania yamekuwa imara, himilivu na yenye mafanikio makubwa, licha ya uwepo wa athari za janga la UVIKO-19 na migogoro ya kimataifa.

Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa Thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji ambayo imeongezeka kwa asilimia 40.8 na kufikia shilingi trilioni 41.7 katika kipindi kilichoishia Aprili 2024, ikilinganishwa na shilingi trilioni 29.62 katika kipindi kilichoishia Aprili 2021.

“Mauzo ya hisa na hatifungani katika Soko la Hisa yameongezeka kwa asilimia 69.4 na kufikia shilingi trilioni 9.7, ikilinganishwa na shilingi trilioni 5.7.

“Thamani ya Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja imeongezeka kwa asilimia 293.4 na kufikia shilingi trilioni 2.09, ikilinganishwa na shilingi bilioni 532.95.”ameeeza Mkama.

Aidha amesema kuwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imetekeleza mikakati ambayo imewezesha kuanzishwa kwa bidhaa mpya na bunifu ambazo zimewezesha masoko ya mitaji Tanzania kuweka ALAMA TANO za Kwanza za kihistoria za mafanikio Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambazo zimewezesha masoko ya mitaji Tanzania kuwa katika ramani ya masoko ya mitaji ulimwenguni yanayotoa bidhaa mpya na bunifu, zinazovutia wawekezaji wa ndani na kimataifa.

Amezitaja bidhaa hizo kuwa ni Hatifungani ya kwanza yenye mguso na matokeo chanya kwa Jamii, yaani social bond iliyotolewa katika fedha mbalimbali Afrika;

Ameitaja nyingine kuwa ni Hatifungani ya kwanza ya kijani yaani green bond yenye thamani kubwa na iliyotolewa katika fedha mbalimbali, Kusini mwa Jangwa la Sahara;

“Hatifungani ya kwanza yenye mguso wa jinsia yaani gender bond, Kusini mwa Jangwa la Sahara,Hatifungani ya kwanza inayokidhi misingi ya Shariah yaani corporate fursa sukuk bond; na

“Hatifungani ya kwanza iliyotolewa na shule ya sekondari ya wasichana na ambayo inakidhi misingi ya Shariah yaani premier sukuku bond.

Related Posts