MR MWANYA ATEMBELEA KIJIJI CHA NGURUWE DODOMA

Msanii mkubwa na Maarufu anayejihusisha na sanaa ya uchekeshaji hapa Nchini almaarufu Mr Mwanya ametembelea Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero Jijini Dodoma kwa ajili ya kujionea uwekezaji mkubwa unaofanywa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Nguruwe Project Simon Mkondya Maarufu kwa jina la Mr Manguruwe.

Msanii huyo pia ameweka wazi juu ya uwekezaji alioufanya katika eneo hilo ambapo amesema mara tu alipobahatika kufahamu habari kutoka katika kijiji hicho cha nguruwe amefanya uwekezaji mkubwa ambao kwa sasa anasema unafikia Milioni 700.

Akiwa katika kijiji hicho Mr Mwanya ameonesha kufurahishwa na uwekezaji alioufanya kwani umeshaanza kumpa faida kubwa ya uwekezaji wake.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mr Mwanya amesema kama Watanzania hususani vijana wataamka na kuanza kufanya uwekezaji huu katika kijiji hicho cha Nguruwe anaamini changamoto ya  kulalamika juu ya ukosefu wa ajira hapa nchini itapungua.

Mkurugenzi wa kijiji hicho, Simon Mkondya ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hapa Nchini na kusema kuwa hii itasaidia sana kuongeza wawekezaji wa ndani na hivyo kuwataka Watanzania hususani Vijana kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika kijiji hicho cha Nguruwe kilichopo katika eneo la Zamahero Nje kidogo ya Jiji la Dodoma.

Msanii mkubwa na Maarufu anayejihusisha na sanaa ya uchekeshaji hapa Nchini almaarufu Mr Mwanya akiwa katika Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero Jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Kijiji cha Nguruwe Project Simon Mkondya Maarufu kwa jina la Mr Manguruwe akionesha moja ya nguruwe waliopo katika kijiji cha Nguruwe

Related Posts