Mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe subira yavuta heri

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri ameongoza ujumbe wa Wizara katika kufanya ukaguzi maendeleo ya Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe ambao kwasasa upo asilimia 88 za utekelezaji.

Mhandisi Mwajuma amefanya ukaguzi katika eneo la chanzo na kujionea jinsi maji yanavyochukuliwa na kusukumwa hadi kwenye chujio la kuchuja maji na maji kusukumwa hadi katika tenki kubwa la usambazaji lililopo kisangara kisha kupelekwa vudoi na kiverenge katika matenki mengine makubwa na kwenda kwa wananchi.

Mwandisi Mwajuma ameweka wazi mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe utakamilika ndani ya kipindi kilichopangwa na kazi kubwa itakayobakia ni kusambaza maji kwasababu kazi kubwa imekwishakamilika katika awamu ya kwanza na ya pili na kazi kidogo sana imebakia.

Katika ujumbe wake Mhandisi Mwajuma ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe. Agness Kisaka Meena ambaye kwa upande wake amewahakikishia wananchi kuwa mradi huu mkubwa ni suluhisho la upungufu wa maji waliokuwa wakiupata wakati wote sasa unakwenda kukamilika.

 

Related Posts