Msimu wa pili tuzo za wanamichezo BMT Juni 9

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Msimu wa pili wa tuzo za wanamichezo bora za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa mwaka 2023 , unatarajia kufanyika Juni 9, 2024, zikihusisha wanamichezo waliofanya vizuri Kimataifa ambapo  jumla ya vipengele 16 vitashindaniwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 15, 2024 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa BMT Leodgar Tenga, amesema   tuzo hizo zina faida  kubwa na lengo ni kuhamasisha na kuchangia maendeleo ya michezo.

Tenga amesema kwa sasa Tanzania ipo juu kimichezo, hilo likidhirishwa na kitendo cha timu mbili za Simba na Yanga kufanikiwa kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunatoa tuzo kwa watu wanaofanya vizuri Kimataifa. Sasa hivi Tanzania si kichwa cha mwendawazimu tena, watu wakija hapa wanajipanga,” ameeleza Tenga.

 Naye Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo hizo, Prof. Madundo  Mtambo amesema  lengo lao ni kuwaenzi na kuwatambua wanamichezo waliofanya vizuri na zitakuwa ni tofauti na zilizopita.

Amesema tuzo zilizopita zilitoa mchezaji bora kila mchezo lakini  wa sasa kutakuwa na mwanamichezo bora wa jumla  ambaye amefanya vizuri kuliko wote na vipengele vingine.

“Vipengele vimeongezeka, pia kutakuwa na tuzo za kocha bora wa mwaka, mwamuzi bora wa mwaka na mwandishi bora wa habari za michezo lengo kuleta ushindani,”amesema.

Amefafanua kuwa mchakato wa utoaji tuzo  hizo unafanyika kwa uwazi, weledi, na umakini  na vyama na mashirikisho yote ya michezo ndiyo yatateua wanamichezo.

 katika uteuzi wa wanamichezo bora katika michezo yao. Kamati ya usimamizi wa tuzo imepokea mapendekezo ya vyama, itayachambua na kuchagua wanamichezo bora.

Related Posts